
Mama wa mtoto aliyeitwa Makambo akiwa na mtoto pamoja na Mwenyekiti wa Matawi ya Yanga mkoani Mbeya
Mtoto huyo ambaye amepewa jina hilo alizaliwa baada ya goli la pili la Makambo katika mchezo huo uliopigwa 29/12/2018 kwenye uwanja wa Sokoine.
Wazazi wa mtoto huyo kwa pamoja walikubaliana kumpatia jina la Heritier Makambo tayari Mwenyekiti wa Matawi ya Yanga mkoa wa Mbeya, Chuma Mahinya, amewatembelea na kuwapa mkono wa pongezi kwa mama wa mtoto.
Heritier Makambo
Katika mchezo huo Makambo alifunga mabao yote mawili ya Yanga katika mchezo huo akianza dakika ya 16 huku lile la pili akifunga dakika ya 41 ya mchezo huo ambao Yanga ilichukua alama tatu.