Jumanne , 31st Mar , 2015

Vijana nchini wametakiwa kushiriki zaidi katika michezo mbalimbali ili kuweza kujipatia ajira ambayo itaweza kuwasaidia katika maisha yao ya kila siku.

Akizungumza jijini Dar es salaam, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda amesema, Vijana wengi wa kitanzania hupanga foleni kwa ajili ya kutafuta ajira bila kujua kuwa kipaji alichonacho ni ajira kwake na inaweza kumsaidia kuliko kuajiriwa.

Makonda amesema, vijana watakapokuwa na vipaji na kuweza kujiajiri kutasaidia hata kupunguza uhalifu au utumiaji wa madawa ya kulevya vitu vinavyopingwa vikali na jamii pamoja na serikali.