Jumapili , 2nd Oct , 2022

Takribaani watu 174 wamepoteza maisha kwenye mapigano yaliyotokea kwenye mechi ya mpira wa miguu huko nchini Indonesia, na kupelekea kuwa janga haya zaidi kuwahi kutokea duniani katika uwanja wa mpira wa miguu. 

Watu wengine 180 walijeruhiwa kwenye ugomvi huo baada ya timu ya nyumbani ya  Arema FC kupoteza mchezo dhidi ya mahasimu wao wakubwa katika uwanja uliokua umefurika Mashabiki wengi huko Malang, Mashariki mwa  Java jana saa za jioni.

Ilikua ni baada ya polisi kuwatawanya mashabiki waliovamia uwanja kwa mabomu na machozi na kupelekea janga Hilo kubwa..

Wakati kundi kubwa lililovamia uwanja likiwa kwenye sintofahamu, maelfu ya Mashabiki walielekea geti la kutokea nje ya uwanja wa  Kanjuruhan ambapo wengi walianguka chini.

Shiirikisho la mpira wa miguu duniani Fifa, huwa haliruhusu maaskari wa serikali kutumia mabomu ya machozi uwanjani.

Rais Joko Widodo amesitisha mechi zote nchini humor mpaka uchunguzi ufanyike