Jumatano , 9th Feb , 2022

Klabu ya Manchester united sasa imeshuka kutoka nafasi ya 4 hadi nafasi ya 5 katika msimamo wa EPL baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 na Burnley usiku wa jana kwenye dimba la Turf Moor. Katika mchezo huo nyota wa Ureno Cristiano Ronaldo alianzia benchi ikiwa ni mechi wake wanne.

(Jay Rodriguez akifunga bao kuisawazishia Burnley usiku wa jana)

Naye kiungo mfaransa Paul Pogba alifunga goli pekee la United ikiwa ni goli lake la kwanza tangu alipofunga mwezi Januari mwaka 2021 katika EPL. Klabu ya West ham United nayo imepata ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Watford na kupanda hadi nafasi 4 katika msimamo wa EPL, huku Newcastle United nao wakipanda hadi nafasi ya 17 baada kupata ushindi wa magoli 3-1 dhidi ya Everton.

Ligi hiyo itaendelea tena usiku wa leo Februari 9, 2022 kwa michezo minne ambapo Norwich City watakuwa nyumbani kuwakaribisha Crystal Palace, na vijana wa Antonio Conte Tottenham Hotspurs watakabiliana na Southampton, huku katika dimba la Etihad Manchester City watakua wenyeji wa Brentford, na Aston Villa watakipiga dhidi ya Leeds United.