
Afisa Muhamasishaji na Msemaji wa Klabu ya Yanga, Antonio Nuggaz (Kushoto) akiwa katika Studio za East Africa Radio kuzungumza na Mashabiki wa Simba na Yanga.
Mvela ameyasema hayo katika kipindi cha michezo cha Kipenga Xtra kinachoruka kila siku ya Jumatatu mpaka Ijumaa saa sita hadi saba mchana, East Africa Radio wakati akizungumzia juu ya kauli zilizotolewa na wasemaji wa vilabu vya Simba na Yanga juu ya sakata la winga Benard Morrison ambaye ameibua sintofahamu ya uhalali wa mkataba wake baina ya Timu hizo mbili watani hapa nchini.
Kwa upande wa Manara alinukuliwa akiitupia lawama Kamati inayoshughulikia sakata la Morrison akidai kwamba linashindwa kutoa haki stahiki,huku Nuggaz akihamasisha kupitia mitandao yake ya kijamii kuwa haki yao haipotei na kuzua taharuki kwa mashabiki.
Mvela amesema sifa ya wasemaji wa Timu ni kujenga mahusiano baina ya Klabu, na Mashabiki pamoja na wafanyabiashara lakini kwa bahati mbaya Haji Manara kwa upande wa Simba na Antonio Nuggaz ambaye ni wa Yanga, wanafanya kazi kwa maslahi yao na baadhi ya watu binafsi.
Amedai kwamba Manara alikingiwa kifua na mmoja ya viongozi wa juu wa Klabu ya Simba ingawa aliyekua Mtendaji Mkuu Senzo Mazingiza alitaka kuajili mtu mwingine,huku kwa Nuggaz akiwa anafanya kazi kwa kuipa nguvu GSM.
Katika hatua nyingine, Mvela amesema kwa kufanya hivyo, inawezekana wasemaji hao wakatengeneza urafiki na baadhi ya kampuni huku yakiwanyima fursa kupata fedha kutoka kwa Taasisi nyingine za fedha jambo ambalo amelitafsiri kama kubomoa mahusiano.
Kumekua na tambo za pande hizo mbili kwenye soka la Tanzania huku wasemaji wakiwa na nguvu kubwa ya kuzungumza na wanachama pamoja na mashabiki, lakini wengi wanatafsiri kuwa wasemaji hao kwa kiasi kikubwa hawafuati miiko ya kazi zao.