(Wachezaji wa Manchester United wakishangilia moja ya bao kwenye EPL)
Michezo miwili iliyopita ya 'The Red Devil' walishinda dhidi ya West Ham kwa bao 1-0 na waliifunga Brentford mabao 3-1, matokeo hayo yamewafanya kufikisha alama 38 wapo nafasi ya 4 na usiku huu wanacheza dhidi ya Burnley ambao wanaburuza mkia kwenye msimamo wa EPL wakiwa na 13 tu kwenye michezo 19.
Rekodi pia zinawababe Manchester kwani kwenye michezo 3 iliyopita dhidi ya Burnley wameshinda yote ikiwemo ushindi wa bao 1-0 kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza. Michezo mingine ya EPL inayochezwa leo ni West Ham United wao wataminyana na Watford na Newcastle United wanakipiga dhidi ya Everton.




