Jumatatu , 14th Oct , 2019

Mshambuliaji wa zamani wa Simba, Emmanuel Okwi amewashukuru wachezaji wenzake wa timu ya taifa ya Uganda, baada ya ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Ethiopia kwenye mechi ya kirafiki huku yeye akifunga goli hilo.

Kikosi cha timu ya taifa ya Uganda.

Okwi amesema anaipongeza timu nzima kwa jitihada nzuri ambazo zimewapa ushindi, na kuwataka wote wafurahie ushindi huo ambao waliupata jana jioni ugenini.

''Timu nzuri kwa jitihada za kila mmoja, tunashukuru na tufurahie ushindi', amesema Okwi.

Okwi sasa ameifungia magoli mawili timu yake ya taifa katika mechi mbili za kirafiki zilizopita, ambapo mchezo wa kwanza ulikuwa dhidi ya Kenya Septemba 8, alipofunga goli dakika ya 23 lakini Keneth Muguna akaisawazishia Kenya dakika ya 51 na mchezo kumalizika kwa sare ya 1-1.

Katika mchezo dhidi ya Kenya Okwi alikuwa nahodha wa Uganda ambayo ilikuwa ikimkosa nahodha wake na mlinda mlango Denis Onyango. Katika mchezo wa jana dhidi ya Ethiopia Onyango alikuwepo.