Jumatano , 9th Feb , 2022

Mwenyekiti wa wawakilishi wa Tanzania kimataifa klabu ya simba Murtaza Mangungu amesema anaamini timu yao itafanya vizuri katika michuanoya kombe la shirikisho barani Africa kwani kikosi chao pamoja na benchi la ufundi limejiandaa vyema na michuano hiyo.

(Mwenyekiti wa Simba SC kwa upande wa Wanachama, Murtaza Mangungu)

Pia Mwenyekiti Mangungu amewasihi mashabiki wa simba na wadau wa soka nchini kujitokeza kwa wingi kununua tiketi ikiwezekana hadi ijumaa wiki hii ziwe zimekwisha, ili waombe shirikisho la soka Africa CAF liwaongezee idadi ya mashabiki wanaotakiwa kuingia uwanjani.

Simba itashuka dimbani majira ya saa 10 jioni siku ya jumapili ya tarehe 13 mwezi huu, kuwakabili Asec Mimosas ya Ivory Coast katika mchezo wao wa kwanza wa hatua ya makundi ya kombe la shirikisho Africa utakaopigwa katika dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Bei za viingilio katika mchezo huo itakua ni 150,000 kwa platnumz, VIP 'A' shilingi 40,000, VIP 'B na C' shilingi 20,000 na mzunguko ni shilingi elfu 5,000.