Jumatatu , 3rd Jun , 2019

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda amekamilisha ahadi yake kwa wachezaji wa Simba waliopata tuzo kwenye Mo Simba Awards, ambapo aliahidi kuwapa fedha.

Aishi Manula

Makonda ametimiza ahadi hiyo leo Mei 3, 2019 ofisini kwake, ambapo ametoa milioni 1 kwa kila mchezaji, isipokuwa mlinda mlango Aishi Manula aliyepata shilingi Mil. 10 huku msemaji wa Simba Haji Manara akitoa Mil. 3 na mchezaji wa Simba Queen, Mwanahamisi Mil. 2.

Makonda aliahidi zawadi hizo ikiwa ni ahadi yake kutokana na walivyojituma kwenye msimu uliopita ambapo walitetea ubingwa wa ligi kuu soka Tanzania bara pamoja na kufika hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Waliopewa zawadi hizo ni:- 

Aishi Manula Mil.10
Haji Manara Mil.3
Mwanahamisi Mil.2
Meddie Kagere Mil.1
Erasto Nyoni Mil.1
John Bocco Mil.1
James Kotei Mil.1
Clatous Chama Mil.1