Katibu mkuu wa timu hiyo, Beno Njovu amesema kuwa matokeo ya sare ya bao 1-1 katika mchezo wa jana dhidi ya Azam fc ni moja kati ya matokeo matatu katika mchezo wa soka, na pia ikumbukwe hata wapinzani nao wanakua wamejiandaa
Njovu amesema kuwa wana uhakika wakutetea kombe hilo na kuwataka mashabiki wa timu hiyo wawape moyo wachezaji ili wakaibuke na ushindi ugenini jumamosi hii dhidi ya maafande wa Rhino ya Tabora mchezo utakaopigwa katika uwanja wa Ally Hassan Mwinyi.