Jumatano , 19th Oct , 2016

Bondia Mtanzania Thomas Mashali amesema, anaamini kambi ya muda mrefu ya maandalizi ya mpambano wake wa kuwania Ubingwa wa WBO dhidi ya Mmalawi Chimwemwe Chiotcha itamsaidia kufanya vizuri katika pambano hilo.

Bondia Thomas Mashali

Mashali amesema, Chimwemwe siyo bondia mbaya na anajipanga vizuri kwa ajili ya mpambano huo kwani mpambano wowote wa ngumi hautabiriki hivyo anaamini maandalizi yake ya safari hii yatasaidia kuweza kuwafurahisha mashabiki wake na Watanzania kwa ujumla.

Mashali amesema, Chimwemwe ni bondia ambaye anafanya vizuri katika kazi zake na huwa anapambana kuhakikisha anaibuka na ushindi lakini kwa safari hii atahakikisha anafanya maandalizi ya kutosha ili kujihakikishia ushindi mbele ya mpinzani wake huyo.

Pambano hilo litapigwa mwezi wa Desemba mwaka huu jijini Dar es salaam.