Jumapili , 30th Mar , 2014

Bondia Thomas Mashali ameshinda Pambano la kuwania ubingwa wa kimataifa wa UBO, dhidi ya bondia Japhet Kaseba kwa pointi baada ya kutambiana kwa muda mrefu, katika ukumbi wa PTA jijini Dar es salaam hapo jana usiku.

Katika mpambano huo wa raundi 10 mabondia hao walionyesha uwezo mkubwa hasa Mashali ambaye alionekana katika raundi za 6 za awali kwamba angeibuka na ushindi wa Knock out lakini hali ikabadilika katika raundi ya 7 baada ya Kaseba naye kuzinduka na kumshambulia Mashali

Na baada ya hapo zikapigwa raundi tatu za mwisho ambazo hazikuwa na mabadiliko makubwa kwani mabondia hao walikua wakishambuliana kwa zamu na baada ya mpambano huo nilizungumza na Bondia Thomas Mashali ambaye awali alitamba kummaliza mpinzani wake katika raundi nne za awali

Naye Japhet Kaseba ambaye watu wengi hawakutegemea kumaliza raundi zote 10 katika mpambano huo amesema uzoefu wa mchezo huo ndio umemfanya asiibuke na ushindi kwani yeye awali alikua akicheza kick boxing na amekubali matokeo hayo.