Alhamisi , 18th Oct , 2018

Kocha msaidizi wa zamani wa Simba Masoud Djuma amesaini mkataba unaodaiwa kuwa wa mwaka mmoja kuifundisha klabu ya AS Kigali inayoshiriki ligi kuu soka nchini Rwanda.

Masoud Djuma

Masoud Djuma ameachana na Simba wiki moja iliyopita baada ya kufikia makubaliano ya kuvunja mkataba na uongozi wa klabu hiyo kwa manufaa ya timu.

Kocha huyo wa zamani wa Rayo Sports ataanza ameanza kazi rasmi leo Oktoba 18, 2018 ambapo atakuwa na kibarua cha kuiandaa timu kuelekea mchezo wa kwanza wa ligi kuu dhidi ya Musanze.

Msimu mpya wa ligi kuu ya Rwanda 2018/19 unaanza rasmi kesho, Ijumaa Oktoba 19, ambapo jumla ya timu 16 zitachuana kuwania ubingwa huo.

Mchezo wa kwanza wa Masoud Djuma akiwa na timu yake hiyo mpya ambayo msimu uliopita ilimaliza katika nafasi ya pili nyuma ya APR utapigwa Jumapili Oktoba 21.