
Kalidou Koulibaly akiwa na Dries Mertens (Napoli) na Mauro Icardi (Inter)
Mchezo huo ambao Napoli ilipoteza kwa bao 1-0, ulimalizika kwa wachezaji wawili wa Napoli, Lorenzo Insigne na mwenyewe Kalidou Koulibaly kupewa kadi nyekundu.
Nyota wa klabu ya Juventus, Christiano Ronaldo ameandika katika ukurasa wake wa Instagram, "katika Dunia na soka pia, nimekuwa nikipenda kuwepo kwa elimu na heshima. Kusiwe na ubaguzi na vitendo vingine kama hivyo".
Nahodha wa Inter Milan, Mauro Icardi ameandika, "nimefadhaishwa na kilichotokea jana (juzi) katika uwanja wa San Siro, tuseme sasa hapana juu ya ubaguzi na unyanyasaji".
Mshambuliaji wa Liverpool, Mohamed Salah ambaye aliwahi kucheza ligi ya Italia, ameandika,"hakuna nafasi ya ubaguzi katika soka na hakuna nafasi ya ubaguzi huo katika sehemu nyingine yoyote ile".
Naye mshambuliaji wa klabu ya Napoli, Dries Mertens ameandika katika ukurasa wake wa Instagram, "wewe ni mmoja wa watu wazuri sana ambao ninawafahamu, nakuomba usibadilike na wala usivunjike moyo juu ya haya yote. Nakuomba tusimame pamoja".
Aidha kufuatia kitendo hicho, klabu ya Inter Milan imepewa adhabu ya kucheza michezo yake miwili bila ya mashabiki katika uwanja wake wa San Siro.