Jumanne , 1st Mar , 2022

Beki wa kati wa Simba anayekipiga kwa mkopo Mtibwa Sugar, Ibrahim Ame, amesema mshambuliaji wa Yanga, Mkongomani, Fiston Mayele ameshindikana huku akisisitiza amemkosesha usingizi.

Mshambuliaji wa Yanga Fiston Mayele

Kauli ya beki huyo imekuja baada ya Mtibwa Sugar kufungwa mabao 2 -0 kwenye Uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro hivi karibuni.

Ame amesema kuwa kabla ya mchezo huo kuanza , alipewa jukumu la kumkaba Mayele kwa lengo la kutofunga, lakini imeshindikana baada ya kumruhusu mshambuliaji huyo kufunga bao.

''Bao hilo alilofunga Mayele, limemfanya akose furaha na amani huku akishindwa kupata usingizi huku akiri kuwa Mayele ni mshambuliaji hatari na wa kuchungwa akiwa uwanjani kutokana na kiwango chake bora'' amesema Ibrahim Ame.

Ame alisajiliwa na Simba msimu uliopita akitokea Coastal Union ya Tanga ambaye msimu huu alitolewa kwa mkopo Mtibwa pamoja na Said Ndemla na Jeremiah Kisubi