Jumatano , 12th Aug , 2020

Kocha wa Klabu ya Paris St Germain , Thomas Tuchel amethibitisha kuwa nyota wake Kylian Mbappe atakuwepo kwenye kikosi chake kitakachoumana na Atalanta ya Italia kwenye mchezo wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya.

Mshambuliaji wa PSG Kylian Mbappe katika heka heka dimbani.

Mbappe aliumia kifundo cha mguu kwenye mchezo wa Coupe de France dhidi ya Saint Ettiene ambao PSG ilishinda kwa bao 1-0 na kutwaa taji hilo.

Kuumia kwa Mbappe kuliarifiwa kuwa angekaa nje ya uwanja kwa wiki tatu na huenda angeikosa michuano hii lakini amepona kwa wakati.

Michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya hatua ya Robo Fainali inafanyikia kwenye ardhi ya Ureno kufuatia Shirikisho Barani Ulaya na Wanachama wake kukubaliana kuepusha janga la COVID-19 na kuyamaliza mashindano kwa wakati.