Alhamisi , 14th Mei , 2015

Uongozi wa Timu ya Mbeya City ya jijini Mbeya umesema mpaka sasa hawana mpango wa kuuza au kununua mchezaji mpaka watakapokaa na kushauriana na Kocha.

Akizungumza na East Africa Radio, msemaji wa klabu hiyo, Dismas Ten amesema, taarifa zinazozidi kuenea juu ya timu hiyo kuwatoa wachezaji kwenda klabu ya Simba sio za kweli kwani kufanya hivyo ni mpaka pale dirisha la usajili litakapofunguliwa na pia kukaa na kushauriana na kocha ni kitu gani anahitaji ili kukiboresha kikosi hicho.

Ten amesema, mpaka sasa hawajapanga kutoa na kuuza mchezaji kwani dirisha la usajili ndilo hutoa ruhusa ya kufanya hivyo na uongozi wa timu hupanga wafanye nini kwa timu hiyo.