Mbwana Samatta ahoji kuhusu TP Mazembe

Jumatatu , 25th Nov , 2019

Mshambuliaji na nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania pamoja na klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji, Mbwana Samatta, amehoji juu ya ubora wa klabu ya TP Mazembe pamoja na wachezaji wa Tanzania wanaocheza huko.

Mbwana Samatta akiwa TP Mazembe

Samatta ametumia ukura wake wa Twitter kuhoji hivyo akieleza kuwa haelewi tatizo liko wapi maana wachezaji wa Tanzania ambao wanacheza TP Mazembe hawazingatiwi.

''Ni TP mazembe imepungua ukubwa au wachezaji wetu wa kitanzania waliopo pale ndo sio wakubwa? naona kama hatuna habari nao ivi'', ameindika Samatta.

Wachezaji wa Tanzania wanaocheza TP Mazembe kwasasa ni Eliud Ambokile pamoja na Ramadhan Singano.

Akiwa TP Mazembe kwa takribani miaka mitano, Samatta alifanikiwa kuwa mshambuliaji hatari Afrika huku akiibuka mfungaji bora wa Ligi ya Mabingwa Afrika na kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa ligi za ndani Afrika mwaka 2016.

Ramadhani Singano (kushoto) na Eliud Abokile (kulia)