Alhamisi , 20th Jul , 2017

Ikiwa imebakia siku moja kuanza kwa mchezo wa kwanza wa nusu fainali ya michuano ya mpira wa kikapu ya Sprite BBall Kings timu ya Mchenga BBall Stars yaanza majigambo yake na kuapa kuwa itawapa kichapo kikali wapinzani wao,

Kikosi cha timu ya Mchenga BBall Stars.

 mchezo utakaochezwa siku ya Jumamosi katika uwanja wa Donbosco Oysterbay Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza nahodha wa timu ya Mchenga BBall Stars Mohamed Yusuph amesema katika hatua hii ya nusu fainali ya michuano ya mpira wa kikapu ya Sprite BBall Kings wamejipanga kuukata mdomo wa wapinzani wao kwa madai kipindi cha droo ya kupanga ratiba ya mashindano walijigamba juu yao.

"Tumejiandaa kuwapa dozi ya kutosha wapinzani wetu wa siku hiyo Flying Dribblers kwa sababu walileta kidogo maneno kwa hiyo tunawaomba mashabiki zetu waje na mbwembwe zote kushangilia timu yetu siku ya Jumamosi jinsi inavyochukua ushindi", amesema Yusuph.

                                           Nahodha wa timu ya Mchenga BBall Stars Mohamed Yusuph

Pamoja na hayo, Yusuph amesema kitu pekee kitakachoweza kumpa mtu sifa ya kuwa mchezaji bora ni pamoja na kuwa na nidhamu ya kutosha katika mchezo wenyewe hasa hasa ya kuwaheshimu waamuzi.