Kikosi cha Yanga kilichoanza jana. Tambwe ni wa kwanza kulia (walioinama).
Kocha wa Yanga Mwinyi Zahera amelazimika kumpumzisha mshabuliaji huyo mazoezi ya leo asubuhi ili kumlinda kiafya aweze kupona vizuri.
Taarifa ya Yanga imeeleza kuwa ''Tambwe anapumzika ili apate muda wa kurejea vyema kiafya kufuatia kupasuka karibu na jicho la kulia na kushonwa nyuzi 5 baada ya kugongana na kipa wa Biashara Nurdin Barora''.

Amissi Tambwe
Katika mchezo huo Yanga iliibuka na ushindi wa penalti 4-5 baada ya kutoka sare ya mabao 2-2 katika dakika 90 za kawaida. Mchezo huo ulichezwa jana kwenye uwanja wa Taifa Dar es salaam.


