Jumanne , 19th Oct , 2021

Mchezaji wa zamani wa klabu ya Kaizer Chiefs na Maritzburg United za nchini Afrika Kusini Lucky Maselesele (41) ameripotiwa kushambuliwa na kuuawa na kundi la watu lililomtuhumu kuiba nyaya za umeme.

Picha ya Mchezaji Lucky Maselesele

Msemaji wa polisi, Luteni-Kanali Mavela Masondo amesmea mchezaji huyo ameuawa siku ya Jumamosi, Oktoba 16 eneo la Tsutsumani huko Alexandra jijini Johannesburg .

Mavela Masondo pia amesema washukiwa wote wamefunguliwa mashtaka ya mauaji ya mwanandinga huyo.