Jumatatu , 22nd Mar , 2021

Hizi ni baadhi ya rekodi za ufungaji mabao zilizowekwa mwishoni mwa wiki iliyopita nchini Hispania, Ujerumani, na Ufaransa

Messi

Mchezaji bora wa Dunia mara 6 Lionel Messi amendeleza moto wake ndani ya kalenda ya mashindano mwaka 2021, baada ya hapo jana kufunga mabao mawili kwenye ushindi wa bao 6-1 walioupata FC Barcelona dhidi ya Real Sociadad, msahambuliaji huyu amehusika kwenye mabao 22 katika michezo 12 ndani ya mwaka huu, amefunga mabao 15 na ametoa pasi za usaidizi wa mabao (assists) 7.

Messi pia ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa Barcelona aliyecheza mechi nyingi zaidi (768) akimpiku kiungo wa zamani wa timu hiyo Xavi Hernandez.

Kule nchini Ujerumani mshambuliaji wa Bayern Munich Robert Lewandowski mabao 3 kwenye ushindi wa mabao 4-0 walioupata dhidi ya VFB Stuttgat kwenye mchezo wa ligi kuu Bundesliga, ni kwa mara ya 4 msimu huu mshambuliaji huyo anafunga mabao 3 kwenye mchezo mmoja yani (Hat-trick).

Lewandowski amefikisha mabao 197 katika mechi 215 za Bundesilga tangu aanze kucheza kwenye ligi hiyo na mabao hayo matatu yamemfanya afikishe mabao 35 ya ligi msimu huu na amebakisha mabao matano kufikia rekodi ya Gerd Muller ya kufunga mabao 40 ndai ya msimu huu lakini pia huu ni msimu wa sita mfululizo anafunga mabao 20 au zaidi .

Mshambuliaji huyo raia wa Polandi hajaifunga timu moja pekee msimu huu katika Bundesilga ambayo ni RB Leipzig ambayo atakutana nayo mwishoni mwa wiki hii.

Robert Lewandowski

Mzee wa matukio na Vimbwanga Louis Suarez mshambuliaji wa Atletico Madrid alifikisha mabao 500 katika maisha yake ya soka kwenye michezo rasmi, baada ya kufunga bao la pekee kwenye mchezo wa ligi kuu hispani La liga dhidi ya Deportivo Alaves.

Suarez raia wa Urugua mwenye umri wa miaka 34 hilo lilikuwa ni bao lake la 19 msimu huu kwenye ligi kuu Hispania La Liga msahambuliaji huyo amewahi kuvichezea vilabu vya Ajax, Liverpool, Barcelona na sasa Atletico Madrid, kwenye ngazi ya vilabu amefunga jumla ya mabao 437 na kwa timu ya taifa kafunga mabao 63. 

Louis Suarez

Kule Ufaransa kinda Kylian Mbappe anayeichezea klabu ya PSG ameendelea kutuma ujumbe juu ya ubora wake wa kufumania nyuavu baada ya kufikisha mabao 100 kwenye ligi kuu Ufaransa French League 1, Mbappe mwenye umri wa maika 22 alifunga bao lake la 99 na 100 baada ya kufunga mabao 2 kwenye ushindi walioupata PSG wa mabao 4-2 dhidi ya Olympiqe Lyon.

Na amekuwa mchezaji mwenye umri mdogo kufikia idadi hiyo ya mabao akivunja rekodi ya iliyokuwa ikishikiliwa na Herve Hevelli aliyeiweka akiwa na Sant Ettiene mwaka 1966.

Kylian Mbappe