Jumanne , 22nd Jun , 2021

Rais wa Klabu ya soka ya Barcelona Joan Laporta,amesema anatamani kuona Cristiano Ronaldo na Lionel Messi wanacheza pamoja tena safari hii wakiwa timu moja.

Cristiano Ronaldo

Laporta ambaye amechaguliwa hivi karibuni kuwa Rais wa Klabu hiyo, amesema anaangalia uwezekano wa kumsajili Cristiano Ronaldo kutoka Juventus kwenda Barcelona kucheza pembeni ya mshindani wake mkubwa wa muda wote Lionel Messi

Cristiano Ronaldo amebakiza mkataba wa mwaka moja ndani ya Juventus huku akitajwa kutofurahia maisha  ndani ya timu hiyo kwa sasa, na inawezekana ikawa inachangiwa na kukosa ubingwa wa ligi pamoja na kutolewa mapema katika mashindano ya klabu bingwa Ulaya.

Kwa mujibu wa Laporta anasema dili ya kumnasa Ronaldo huwenda ikaambatana na kubadilishwa kwa wachezaji watatu zaidi Antoine Griezman,Phillipe Coutinho

Laporta alizungumzia pia imani yake ya kumbakiza Messi ndani ya Barcelona licha ya hofu ya mkataba wake kumalizika juni 30/2021

Messi na Ronaldo ni washindi wa Ballon d’or mara 11 kwa pamoja , moja akitwaa tuzo hizo mara 6 na mwingine akitwaa tuzo hiyo mara