Jumanne , 27th Apr , 2021

Mashindano ya mchezo wa Gofu kwa wachezaji wa Kulipwa yanatarajiwa kufanyika April 30 mwaka huu katika Viwanja vya Gofu Lugalo Jijini  Dar es salaam ambayo yatashirikisha vilabu mbalimbali vya mchezo huo hapa nchini.

Msemaji wa Klabu ya Gofu Lugalo Kapteni Selemani Semunyu.

Msemaji wa Klabu ya Gofu Lugalo Kapteni Selemani Semunyu amesema mpaka sasa wachezaji 25 wa kulipwa wameshajiandisha kwa ajili ya mashindano hayo ambapo anaamini katika siku 3 zilizobakia wataongezeka wachezaji wengine.

''Ni mashindano ambayo  yanakuwaga na msisimko mkubwa kwa washiriki kutambiana na hatmae kumpata bingwa ambae atajinyakulia  zawadi huku lengo la kufanya michuano hiyo ni kutambua mchango wa wachezaji wa kulipwa '' amesema msemaji wa klabu ya Gofu Lugalo Kapteni Selemani Semunyu. 

Ameongeza kuwa mashindano pia yatashirisha wachezaji wa ridhaa ikiwa ni sehemu ya mkakati wa klabu Gofu Lugalo kukuza viwango vya wachezaji na kufuata utaratibu wa matukio ya kalenda ya mwaka ya klabu hiyo.

Baadhi ya wachezaji wa kulipwa wa ridhaa kutoka klabu hiyo wameeleza namna ambayo wamejipanga kutoa ushindi kwenye mashindano hayo ambayo yatafikia tamati Mei Mosi mwaka huu.