Andrew Kapelela - Mwenyekiti wa Chama cha Mieleka nchini AWATA
Mwenyekiti wa Chama cha Mieleka nchini AWATA Andrew Kapelela amesema, mara baada ya kumalizika kwa mashindano ya kumuenzi baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere yanayofahamika kama Nyerere Cup wanajipanga kwa ajili ya Mkutano Mkuu wa Mwaka utakaofanyika mwishoni mwa mwezi huu.
Amesema baada ya hapo watakuwa na mashindano ya Klabu bingwa Taifa ambayo yatakuwa ni ya kufunga mwaka yanayotarajiwa kufanyika mwezi wa Desemba mwaka huu.
Kapelela amesema, mashindano ya klabu bingwa Taifa pia yatasaidia kuweza kupata timu bora ya Taifa itakayoweza kushiriki katika mashindano mbalimbali hapo mwakani.