Wachezaji wa timu ya taifa ya Misri wakishangilia baada ya mwamuzi kumaliza mchezo
Timu hizi zilifika hatua ya kupigia mikwaju ya penati ili kumpata mshindi baada ya timu hizi kutoka suluhu 0-0 ndani ya dakika 120. Katika upigaji wa penati hizo wenyeji Cameroon walikosa penati 3 kati ya 4 ambapo walipata penati ya kwanza na wakakosa 3 zilizofata wakati Misri walipata penati zao zote 3 ambazo walipiga na kumfanya mwamuzi Bakary Gassama wa Gambia kumaliza mchezo zikiwa zimepigwa penati 7 tu.
Wachezaji wa Cameroon waliokosa penati ni Clinton Nje, James Lea Siliki na Harould Moukoudi na nahodha Vincent Aboubakar alifunga penati moja, wachezaji wa Misri waliofunga penati ni Ahmed Sayed Zizo, Mohamed Abdelmonem na Mohanad Mostafa.
Misri wanakata tiketi ya kucheza fainali yao ya 10 ya michuano hii ya mataifa barani Africa wakiwa wameshinda ubingwa wa michuano hii mara 7 katika fainali 9 walizocheza mpaka sasa. Kwenye mchezo wa fainali wataminyana na timu ya taifa ya Senegal ambao hawajawahi kushinda ubingwa wa michuano hii na ni kwa mara ya tatu wanafuzu kucheza fainali ya AFCON. Mchezo wa fainaili unachezwa Jumapili Februari 6, 2020,




