Mo Dewji ajibu kuhusu kujiondoa Simba

Alhamisi , 4th Jul , 2019

Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi wa Simba ambaye ni mwekezaji wa timu hiyo, Mohammed Dewji, amejibu taarifa kuhusu kujiondoa Simba.

Mo Dewji

Taarifa hizo zilianza kusambaa usiku wa jana katika mitandao ya kijamii, lakini mwenyewe amejitokeza na kuweka bayana kinachoendelea.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Mo Dewji amesema, "watu wenye nia mbaya. Kazi yao sio kujenga, ni kuvunja tu. Kaa nao mbali. Narudia kaa nao mbali sana!".

Hii leo, Julai 5, katika kurasa zake za mitandao ya kijamii, Mo Dewji ametoa ujumbe mwingine unaoelezea kile kinachoendelea hivi sasa ndani ya klabu hiyo.