Jumapili , 9th Nov , 2014

Moshi Kalsa ya mjini Moshi wameibuka mabingwa wa michuano ya Mpira wa Magongo ya Kombe la Nyerere lililomalizika leo mjini Moshi.

Akizungumza na East Africa Radio, Katibu msaidizi wa Chama cha Mpira wa Magongo Tanzania THA, Mnonda Magani amesema Kalsa imechukua kombe baada ya kuifunga magereza kwa njia ya penati ya goli Tatu ambapo mchezo huo ulianza kwa timu hizo kutoa sare ya goli 2-2 na waliongezewa muda wa ziada ambao hawakufunganana.

Magani amesema michuano hiyo ilitakiwa kuanza Novemba 07 lakini kutokana na jitihada za chama za kutaka kukuza mchezo huu hadi mashuleni waliona ni vizuri kuwa na timu za shule katika michuano hiyo lakini timu hizo zilikuwa na ratiba za mitihani hivyo wakaamua michuano hiyo ianze Novemba 06 ili kuzipa nafasi shule hizo kuendelea na mtihani Novemba 07.