Jumatano , 24th Feb , 2016

Kocha wa zamani wa klabu ya Chelsea Jose Mourinho amesema hajui kocha ajaye wa Manchester United, lakini anatumaini kurudi kwenye benchi la ufundi msimu ujao kama kocha.

Kocha wa zamani wa Klabu ya Chelsea Jose Mourinho amesema hajui kocha ajaye wa Manchester United, lakini anatumaini kurudi kwenye benchi la ufundi msimu ujao kama kocha.

Mourinho mwenye umri wa miaka 53, alitimuliwa na Chelsea mwezi Desemba mwaka jana, ikiwa ni miezi 7 pekee tangu aipe ubingwa klabu hiyo ya jijini London.

Akiulizwa endapo atamrithi Luis Van Gaal Old Trafford, Mourinho alisema: "Hilo ni swali la dola milioni moja". Akimaanisha ni swali kila siku anaulizwa kuhusu kujiunga na Manchester United.

Akiongea eneo la shule moja huko Singapore, aliongeza kwa kusema: "Hakuna anayejua na mimi ni wa kwanza nisiyejua. Nasoma mambo mengi tofauti."

Lakini akongeza: "Kuanza msimu ujao na klabu mpya ni kitu kizuri kwangu."

Mourinho amekuwa akihusishwa kurejea kwenye ligi ya Serie A kujiunga na klabu yake ya zamani ya Inter Milan na kwenye la liga nchini Hispania kujiunga na Real Madrid.

Van Gaal amekuwa katika tanuri la moto ndani ya United, kutokana na timu hiyo kuwa na matokeo mabaya kwenye ligi na mechi za kimataifa, hivyo kuna uwezekano akakatishiwa mkataba wake unaomalizika msimu ujao.

Kocha anayetajwa sana kuchukua nafasi hiyo ni Mourinho na tayari kuna taarifa za chini kwa chini kuwa wawakilishi wa Mourinho wameshafanya mazungumzo na uongozi wa Manchester United.