Jumapili , 23rd Mar , 2014

Bondia Kalage Suba wa Dar es salaam ambaye hivi karibuni ameteuliwa kuchuakua nafasi iliyoachwa w

Bondia Kalage Suba wa Dar es salaam ambaye hivi karibuni ameteuliwa kuchuakua nafasi iliyoachwa wazi na bondia Fadhili Awadhi aliyefariki dunia wiki iliyopita yuko katika maandalizi mazito akijifua kwa ajili ya pambano la March 29 dhidi ya bondia Alan Kamote toka Tanga ukiwa ni mpambano wa ubingwa wa kimataifa wa UBO Afrika.

Kalage amewaondoa shaka mashabiki wake kwamba wasiwe na wasiwasi juu yake kutokana na taarifa za kupewa nafasi ya kucheza pambano hilo kuja kwa ghalfa, kwani yeye kama mwanamichezo ni kama yuko vitani na amekua akijifua kila siku na ujio wa pambano hilo ni suala dogo kwake.

Aidha Kalage ameongeza kwa kusema kuwa pambano hilo ambalo alikua apigane marehemu Fadhili Awadhi ni kama deni kwake na anachotakiwa kufanya ni kushinda ili kumwekea heshima marehemu Awadhi ambaye alikua akipewa nafasi kubwa ya kushinda pambano hilo.