Jumamosi , 25th Jan , 2020

Mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania na Klabu ya Difaa El Jadida ya Morocco, Simon Msuva ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa Klabu yake kwa msimu 2019.

Simon Msuva akikabidhiwa tuzo ya Mchezaji bora

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Simon Msuva ameishukuru uongozi wake wa Klabu ya Difaa El Jadida na kuwataka Watanzania waendelea kumuombea.

"Kwanza kabisa napenda kumshukuru mwenyewezi Mungu mwingi wa rehema na baraka kwa kuniwezesha kufika hapa nilipo toka safari yangu ya mpira mpaka leo naona uwepo wake juu yangu." ameandika Msuva

"Napenda kuwajulisha kuwa kijana wenu leo nimepokea tuzo ya mchezaji bora wa msimu 2019 wa Klabu yangu na sio kwa ujanja wangu bali ni Mungu na nyie ndugu zangu mnaonipa sapoti kwa hali na mali."