(Andy Murray akiwa anashangilia ushindi kwenye Australian Open 2022)
Murray (34) ambaye hakuwa katika kiwango bora tangu afanyiwe upasuaji wa nyonga mwaka 2018 na 2019, amerejea katika nafasi ya 95 kwa viwango vya ubora duniani Jumatatu Februari 9, 2022 tangu mwezi Mei mwaka 2018.
Kwa sasa ananolewa na mkufunzi wake wa zamani Mvenezuela Daniel Vallverdu kwa mkataba wa muda mfupi.
Vallverdu anakumbukwa kwa kumuongoza Murray kutwaa medali ya dhahabu ya Olympic mjini London mwaka 2012, ubingwa wa wazi wa Marekani (US open 2012 ) na ubingwa wa Wimbledon mwaka 2013 huku akiwa na mkataba wa kumfundisha Mswizi Stan Wawrinka ambaye ana majeraha.
Murray sasa atakumbana na Mcanada Felix Auger-Aliassime ambaye anakamata nafasi ya tatu kwa viwango vya ubora Duniani ambaye hapo awali alimtoa Mbelarus Egor Gerasimov kwa seti 2-1.

