Jumanne , 20th Nov , 2018

Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni, ameibua mjadala mkubwa mtandaoni baada ya kuwataka vijana wake wanaocheza timu ya The Cranes kuifunga Tanzania kwenye mechi ijayo ya fainali za kufuzu AFCON.

Kwenye ukurasa wake wa twitter Museveni ameandika ujumbe huo wa kuwatakia kila la heri The Cranes, akisema kwamba licha ya kwamba timu hiyo imeshafuzu kucheza fainali za AFCON, lakini wahakikishe kuwa hawapotezi mechi yao dhidi ya Tanzania.

Kauli ya Museveni ilimfanya Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Zuberi Kabwe kuibuka, na kumtaka Museveni kuacha roho mbaya na kutoibania Tanzania, huku akimkumbusha kuwa mafuta yao yanapita nchini Tanzania.
 

Timu ya Taifa ya Tanzania inatarajia kucheza na The Cranes ya Uganda mwezi Machi, 2019, ambapo iwapo itashinda itakuwa wamepata tiketi ya kushiriki michuano ya AFCON, ambayo inatarajia kufanyika mwaka 2019 nchini Camerron.