
Hassan Mwakinyo akiwa mazoezini.
Mwakinyo ambaye anashika nafasi ya kwanza Barani Afrika kwa sasa, ametoa Rai
akisema wadau wa masumbwi Tanzania wanauchukulia kirahisi mchezo huo kwa kuweka ubishi usio na maana, kwa lengo la kujiridhisha nafsi zao.
Amesema umefika wakati kila mdau anapaswa kufahamu masumbwi ni mchezo wa ajira kama ilivyo michezo mingine duniani, na Bondia anapaswa kupambana kwa malengo ya kujiingizia kipato.
“Duniani kote sijawahi kusikia mabondia wanashindania magari, huwa wanapewa mikanda yenye thamani na pesa ndefu ambazo zitawafanya wanunue magari wanayotaka au wakawekeze kwenye viwanda vya magari baada ya pambano.”
“Mapromota wa Tanzania waupe thamani mchezo huu wa boxing.” amesema Mwakinyo
Mwakinyo anatarajia kupanda ulingoni Kesho kutwa Ijumaa Septemba 3 mwaka huu, kuzichapa na Bondia kutoka Namibia Julius Indongo.
Pambano hilo litafanyika katika ukumbi wa Ubungo Plaza jijini Dar es salaam.