Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Mwakyembe aiomba Taifa Stars

Jumapili , 18th Nov , 2018

Yamebaki masaa machache kushuhudia taifa la Tanzania likiweka historia nyingine itakapovaana na Lesotho jioni ya leo, historia ambayo haitofutika milele endapo timu ya taifa Taifa Stars itapata alama tatu zitakazoipeleka michuano ya AFCON nchini Cameroon mwakani.

Dkt.Harrison Mwakyembe na Taifa Stars

Taifa Stars iliyo katika kundi L, inashika nafasi ya pili kwa alama 5 nyuma ya kinara Uganda yenye alama 13 baada ya kushinda  mchezo wa jana na kujikatia tiketi ya kufuzu michuano hiyo. Nafasi ya tatu ikishikiliwa na Cape Verde yenye alama 4 na Lesotho ikiburuza mkia kwa alama 2.

Stars inahitaji kushinda mchezo wa leo ili kujihakikishia nafasi ya kufuzu AFCON mwakani, ambapo itafikisha jumla ya alama 8 ambazo hata ikipoteza mchezo wake wa mwisho dhidi ya Uganda haitoweza kufikiwa na Cape Verde ambayo itakuwa na alama 7 endapo itashinda mchezo wake wa mwisho dhidi ya Lesotho.

Akizungumza kuelekea mchezo huo, Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe ameitaka Taifa Stars kutowaangusha watanzania zaidi ya milioni 50 ambao leo wako nyuma yao katika mchezo huo.

"Ile hali tuliyoionesha wakati tunacheza na Cape Verde nyumbani tuioneshe sasa, tena iwe mara mbili, watanzania ziadi ya milioni 50 wako nyuma yenu wanawaangalia. Nawaomba sana!! sana!! tena sana!! Taifa Stars tusimuangushe Rais Magufuli," amesema.

"Hawa wenzetu kisaikolojia wameshashindwa toka mwanzo, nadhani matokeo yao hayakuwa mazuri sana kwahiyo hawana matumaini makubwa ya kusonga mbele. Lakini watu kama hawa ndio wachafuzi wakubwa katika juhudi za wengine kusonga mbele, tuingie humo tukiwa tunajua tunapigana na Cape Verde 'B'," ameongeza.

Ikumbukwe Taifa Stars imeshiriki mara moja pekee katika michuano ya mataifa ya Afrika, ambayo ni mwaka 1980 nchini Nigeria. Nafasi ya mwaka huu ni nafasi pekee ambayo itaweka historia kwa mara ya pili kushiriki michuano hiyo baada ya takribani miaka 38.
 

HABARI ZAIDI

Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro SACP Alex Mkama, akionesha vitu vilivyokuwa vimeibiwa

Fundi ujenzi mbaroni mauaji ya dada wa kazi

Wahitimu wa Mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa JKT

Wahitimu JKT watakiwa kulinda miradi ya serikali

Daktari wa GGML aliyebobea katika magonjwa yatokanayo na kazi, Cretus Karwan akimpatia vipimo mmoja wa wananchi waliotembelea banda la GGML na kupatiwa huduma za awali za upimaji wa afya katika maonesho ya OSHA yanayoendelea jijini Arusha.

Wananchi 200 wapimwa afya maonesho ya OSHA

Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Tumaini Nyamhoka akipokea zawadi kutoka kwa Ofisa Mwandamizi wa masuala ya jamii na maendeleo ya kiuchumi kutoka GGML, Ruth Mharagi alipotembelea banda la GGML katika maonesho ya afya na usalama mahali pa kazi jijini Arusha.

TUCTA, OSHA wataka kampuni za madini kuiga ubunifu

Mwili wa Boaz Sanga, Mwanafunzi wa CHuo cha SAUTI Mwanza baada ya kupatikana Pembezoni wa Ziwa Viktoria

Mwanafunzi wa SAUTI afariki akijaribu kuogelea

Luteni Jenerali Charles Muriu Kahariri, CDF Mpya wa Kenya

Luteni Charles Muriu ateuliwa kuwa CDF mpya Kenya

Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe

Taifa limejitosheleza kwa chakula kwa 124%

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda (Mwenye shati ya Bluu) akipata maelekezo wakati wa maonesho ya OSHA 2024 kwenye Viwanja vya General Tyres jijini Arusha.

RC ataka GGML iboreshe maisha ya wananchi Geita