Jumatatu , 21st Aug , 2017

Ikiwa zimebaki siku kadhaa kuendelea kwa vita kali ya aina yake katika fainali za Sprite BBall Kings kati ya TMT dhidi ya Mchenga BBall Stars, EATV imeliweka hadharani kombe linalogombewa.

Vikombe vya washindi wa michuano ya Sprite BBall Kings.

EATV imechukua uamuzi huo baada ya kubaki mechi mbili kupatikana kwa mshindi wa michuano hiyo, japo mpaka sasa mashabiki wa timu ya Mchenga BBall Stars wamejiwekea matumaini ya kuchukua kikombe hicho katika 'game 4' inayotarajiwa kuchezwa Agosti 26 mwaka huu katika viunga vya Don Bosco Oysterbay 

TMT na Mchenga BBall Stars ni timu zilizoweza kuonyesha upinzani mkali tokea kuanza kwa michuano hii jambo ambalo huenda fainali hizi zikaendelea mpaka 'game 5' 

Kikombe atakachokabidhiwa mchezaji bora pamoja na kitita cha fedha taslimu Milioni 2.

Mechi hiyo ya game '4' siku ya Jumamosi Agosti  26 itarushwa mubashara kupitia tinga namba moja kwa vijana EATV pamoja na East Afrika Radio tokea viwanja vya Don Bosco Oysterbay.