Jonasia akikabidhiwa funguo na Rais Malinzi
Taarifa ya TFF imesema kuwa wadau kadhaa wa mpira wa miguu, wamemzawadia gari Jonesia Rukyaa mwamuzi mwandamizi wa FIFA ambaye alipangwa kuchezesha michuano hiyo iliyomalizika kwa timu ya wanawake ya Nigeria kuibuka na ubingwa.
Jonesia, ambaye amepata pia kuchezesha mchezo wa watani wa jadi katika soka nchini, alichezesha mechi ya awali na kuonekana kutokuwa na upungufu kwenye kutafsiri sheria 17 za soka.
Alipangwa kuchezesha mechi ya mshindi wa tatu kati ya Ghana na Afrika Kusini.
Rais wa TFF Jamal Malinzi (kulia) akimkabidhi zawadi mwamuzi Jonasia Rukyaa