
Rais Karia ametoa pongezi hizo leo na kueleza kuwa ushindi wa Dr.Ndumbaro unaongeza idadi ya wanamichezo ndani ya bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambao wanaweza kuwa chachu ya maendeleo ya michezo hususani mpira wa miguu.
“Tunaamini uwezo wa Dr.Ndumbaro katika uongozi tumemuona katika mpira wa miguu akiongoza katika sehemu mbalimbali hakika uwezo wake wa uongozi ni mkubwa na atasaidia sana kukua kwa sekta hii ya michezo'', amesema Karia.
Dr.Ndumbaro amewahi kushika nafasi mbalimbali za uongozi kwenye mpira wa miguu na hivi karibuni Rais Karia alimteuwa kuwa mwenyekiti wa kamati ya rufaa ya leseni za klabu.
Dr.Ndumbaro aligombea katika Jimbo la Songea Mjini kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kushinda kwa kura 45762 akiwazidi wagombea wengine 7 kutoka vyama mbalimbali.