
Makao Makuu ya klabu ya Yanga
Taarifa hiyo ilitolewa na Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini la klabu hiyo ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Mkuchika, Novemba mwaka uliopita kufuatia sintofahamu juu ya uchaguzi mkuu wa klabu hiyo.
Mkuchika alisema kuwa, Manji aliliambia Baraza la Wadhamini la klabu ya Yanga kuwa tarehe ya leo ndipo atakapoanza kwenda katika ofisi yake ndani ya makao makuu ya klabu hiyo, alipokuwa akijibu barua ambayo aliandikiwa na Baraza hilo.
Ikumbukwe kuwa mchakato wa uchaguzi wa klabu hiyo umesimamishwa na Mahakama kufuatia baadhi ya wanachama kushtaki juu ya mwenendo mzima wa uchaguzi huo ambao ulitakiwa kufanyika wikiendi iliyopita.
Mashabiki na wanachama wa Yanga, wanasubiri endapo Mwenyekiti wao wa zamani, Yusuph Manji atarejea katika nafasi yake hii leo ama la!.