Jumamosi , 4th Jan , 2020

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Mh Damas Ndumbaro, ambaye ni shabiki mkubwa wa klabu ya soka ya Simba na amewahi kuiongoza kwa nyakati tofauti, amesema timu yake hiyo ina nafasi kubwa ya kushinda kwenye mchezo wa leo.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Mh Damas Ndumbaro

Akiongea na EATV, Ndumbaro amesema Simba kwasasa ina kikosi kizuri na kinaweza kucheza na timu yoyote na pia ipo katika hali nzuri kiuchumi hivyo ina kila sababu ya kushinda pambano la watani wa jadi.

'Unajua Simba wana viwanja vyao vya mazoezi hivi sasa lakini Yanga bado wanahangaika mpira umewashinda wanahangaika na vifusi pale kwao na mafuriko haya unaweza kufuga hata kambale pale, kwahiyo tarehe 4 ni msiba mkubwa', amesema.

Mchezo huo ni wa kwanza kwa watani wa jadi msimu huu, ambapo utapigwa leo kwenye uwanja wa Taifa Dar es salaam kuanzia saa 11:00 jioni.

Simba kwasasa wanaongoza ligi wakiwa na pointi 34 kwenye mechi 13 huku tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa ni 24. Yanga wapo nafasi ya 3 wakiwa na pointi 24 kwenye mechi 11 na wastani wa magoli ya kufunga na kufungwa ni 6.