Ijumaa , 31st Dec , 2021

Klabu ya soka Namungo FC, imemtambulisha benchi jipya la ufundi baada ya kuondoka kwa Hemed Morocco na Msaidizi wake Geofrey Okoko ikiwa ni makubaliano ya pande zote mbili.

Na sasa kibarua hiko cha kocha Mkuu kitakuwa chini ya Hanoor Janza raia wa Zambia akisaidiana na Jamhuri Kihwelo raia wa Tanzania kama kocha msaidizi.

Namungo licha ya kufanya usajili wa wachezaji 13 kutoka nje mpaka ya je, bado imekuwa ikisusua kwenye ligi kuu ya NBC, wakishinda michezo mitatu tu pekee mpaka sasa, huku wakifungwa mitanange minne na sare nne.

Kibarua cha kwanza kwa kocha Hanoor ni kuhakikisha wanashinda michezo wao wa kwa unayofuata dhidi ya Polisi Tanzania kwenye uwanja wa Ushiriki siku ya Tarehe 14, Januari 2022.