Alhamisi , 26th Aug , 2021

Tuzo ya mchezaji bora wa ulaya mwaka 2021 inayotolewa na shirikisho la soka barani humo UEFA inatolewa leo usiku Agosti 26, 2021, katika hafla itakayofanyika Istanbul nchini Uturuki. na tuzo zitakazo tolewa ni tuzo ya kocha bora na mchezaji bora.

Kevin De Bruyne, N’Golo Kanté na Jorginho wanawania tuzo ya mchezaji bora wa mwaka.

Wachezaji wanaowania tuzo ya mchezaji bora ni Ngolo Kante wa Ufaransa na klabu ya Chelsea, Jorginho wa Chelsea na timu ya taifa ya Italia pamoja na Kelvin De Bruyne wa Mancheater City raia wa Ubeligiji, wachezaji wote hawa wanatoka katika idara ya kiungo.

Kwa upande wa makocha wanoa wania tuzo ya kocha bora wa mwaka ni Thomas Tuchel ambaye alikiongoza kikosi cha Chelsea kutwaa klabu bingwa Ulaya, Pep Guardiola wa Manchester City aliiwezesha The Citizen kushinda ubiungwa wa Ligi kuu England na kocha mwingine anaewania tuzo hii ni Roberto Mancini wa timu ya taifa ya Italia ambaye alikiongoza kikosi cha Azzurri kutwaa ubingwa wa mataifa barani ulaya kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1968.

Tuzo nyingine zitakazo tolewa ni ile ya Mshambuliaji bora ambayo inawaniwa na Erling Haaland wa Borussia Dortmund,, Kylian Mbappé wa Paris Saint-Germain na mshambuliaji wa Bayern Munchen Robert Lewandowski.

Wanaowania tuzo ya kiungo bora ni Kevin De Bruyne wa Manchester City FC, Jorginho wa Chelsea FC, N’Golo Kanté nae kutoka Chelsea FC.

César Azpilicueta, Antonio Rüdiger kutoka Chelsea na Rúben Dias wa Manchester City hawa wanawania tuzo ya beki bora na kwa upande wa golikipa bora wanao wania ni Thibaut Courtois wa Real Madrid Ederson kutoka Manchester City na Édouard Mendy wa Chelsea.