Jumanne , 23rd Dec , 2025

Baada ya kuinusuru Santos FC isishuke daraja katika Ligi ya Brazil, mshambuliaji, Neymar anatarajia kufanyiwa upasuaji.

Nejmar Jr

Akiwa na Santos FC, Neymar alicheza mechi tatu akiwa na jeraha, akafunga mabao manne na kutoa pasi moja ya bao .

Atafanyiwa upasuaji na daktari wa timu ya taifa ya Brazil Rodrigo Lasmar, huku shirikisho la soka nchini humo (CBF) likifuatilia kila hatua .

Hii ina maanisha kuwa, huenda mshambuliaji huyo, akawa sehemu ya kikosi c ha Brazil wakati wa fainali za Kombe la Dunia 2026, endapo upasuaji wake utafanikiwa kwa 100%