Alhamisi , 28th Apr , 2022

Bondia wa uzani mzito anayeshikilia mkanda wa WBC kutoka Uingereza, Tyson Fury ameweka wazi dhamira yake ya kustaafu mchezo wa masumbwi baada ya kumtwanga Dillian Whyte siku ya Jumamosi kwa KO kwenye round ya sita.

Fury ambaye anashikilia rekodi ya mapambano 33, akishinda 23 kwa njia ya Knock-out katika mapambano 32 aliyopanda ulingoni huku akitoa sare 1 dhidi ya Deontey Wilder.

Bingwa huyo wa WBC amesema kuwa anafuraha kuwa anastaafu ndoni akiwa na nguvu, afya njema huku bado akiwa na uwezo mzuri wa kuchanganua maswala muhumi akiwa na utimamu mkubwa.

"Mchezo wa masumbi ni mchezo wa hatari sana, unaweza kuangushwa kwa ngumi moja tu, kama tulivyoshuhudia siku ya jumamosi, ukipigwa ngumi moja nzito unajikuta upo chini umedondoka na unaweza usiinuke tena kuendelea na pambano"

"Na sasa natazamia kustaafu, huu ni ukweli, ukweli kama ule wa injili kuwa sasa rasmi naachana mchezo wa masumbwi, nina mke mzuri, watoto sita, nina mafanikio mengi na umaarufu, nini tena ninachotafuta?" alisema Fury.

Pambano la Jumamosi katika uwanja wa Wembly mbele ya mashabiki 94,000 imetoa taswira kuwa ni pambano la mwisho kwa Fury ambaye anastaafu akiwa hajapoteza pambana kama ilivyo kwa bondia wa zamani wa Marekani, Rocky Marciano aliyestaafu na rekodi ya mapambano 49 akishinda 43 kwa njia ya Knock-out.