Alejandro Garnacho
Garnacho, aliyenunuliwa kwa Pauni 40M akitokea Man United, amekuwa na wakati mgumu kwani hadi sasa amefunga mabao manane tu msimu mzima (manne yakiwa dhidi ya timu ndogo kama Wrexham na Port Vale), huku akitoa asisti nne pekee.
Sababu nyingine iliyotajwa ni kiwango duni alichokionyesha dhidi ya waajiri wake wa zamani, Man United wakati wa mechi ya EPL wikiendi iliyopita.
Mambo yamezidi kuwa mabaya baada ya Luke Shaw na Bruno Fernandes kuonekana kumbeza mtandaoni, huku kitendo chake cha kufuta picha za Chelsea kwenye TikTok kikiamsha hasira za mashabiki na mabosi wa klabu.



