Haruna Niyonzima (katikati)
Niyonzima ambaye alifanya kazi kubwa ya kusaidia kupatikana kwa bao la ushindi la Simba ambalo liliwapeleka robo fainali ya Ligi ya mabingwa Afrika, amesema siku zote alikuwa na ndoto hiyo hivyo hakutaka kuiacha.
''Niliumia lakini nikajiambia siruhusu hili linikwamishe, sikutaka kuwaangusha mashabiki na kocha kwa kuniamini ukizingatia nilifanya maandalizi ya muda mrefu kwaajili ya siku moja kufanya kitu kama hicho, hivyo nakiri Machi 16, 2019 ilikuwa siku yangu kubwa kwenye soka ngazi ya vilabu'', - Amesema Niyonzima.
Aidha amemshukuru kocha wake Patrick Aussems kwa kumwamini na kumpa dakika chache za kutimiza malengo yake. Niyonzima aliingia kipindi cha pili akichukua nafasi ya Emmanuel Okwi.
Niyonzima amemaliza kwa kusema kuwa baada ya kufika robo fainali sasa anaamini kuwa, wanayo nafasi ya kufika fainali na kikosi chao kinauwezo huo kwa kuzingatia wingi wa mashabiki walionao.
Simba imetinga hatua ya robo fainali Jumamosi Machi 16, 2019 baada ya kuifunga AS Vita mabao 2-1 na kufikisha alama 9 nyuma ya Al Ahly yenye pointi 10 kwenye kundi D.