Jumanne , 27th Nov , 2018

Mlinzi wa kushoto wa klabu ya Yanga Gadiel Michael amefanyiwa vipimo leo, ambapo daktari wa Yanga Dr. Bavu amesema anaendelea vizuri.

Kikosi cha Yanga

Akiweka bayana hali ya Gadiel ambaye aliumia kwenye ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mwadui FC alhamis iliyopita, Dr. Bavu amesema anaelekea kupona na hali yake ni nzuri kwasasa.

''Gadiel anaendelea vizuri, tumemfanyia vipimo na hakuna shaka kuwa wakati wowote anaweza kurejea uwanjani'', amesema Dr Bavu.

Gadiel Michael ni mmoja wa wachezaji wawili wa Yanga ambao walitoka kwenye timu ya taifa iliyocheza na Lesotho na kuunganisha kwenda kucheza dhidi ya Mwadui pamoja na Feisal Salum huku nyota wengine Kelvin Yondani na Beno Kakolanya wakiikacha timu hiyo.

Yanga ilicheza michezo miwili mkoani dhidi ya Mwadui na Kagera Sugar na kuibuka na ushindi katika michezo yote hivyo kujiweka vyema kwenye msimamo wa ligi wakishika nafasi ya 2 na alama 32.