Alhamisi , 7th Jul , 2022

Kampuni ya michezo ya bahati nasibu Parimatch imeamua kutoa fursa ya kipekee kwa wateja wake wote kwa  kuwapa fursa ya kijanja ya Uwakala, inayowezesha washiriki wa mchezo wa kubahatihsa kugawiwa kiasi cha asilimia 25 ya faida kampuni inayoipata.

Tukio la Parimatch kugawa fursa kwa wateja wake

Hayo yamebainishwa  na Afisa Habari na Mawasiliano wa Parimatch Tanzania, Ismael Mohamed wakati alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari katika maonesho ya Sabasaba hii leo na kusema kwamba, wamechukua maamuzi hayo kwa lengo la kutaka kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya sita katika kupambana na utoaji wa fursa kwa vijana.

Parimatch tumeamua kutoa fursa kwa vijana wa Kitanzania, kwa kutengeneza pesa kiurahisi muda wowote na mahali popote kwa kuwa wakala wetu. Inawezekana kutumia Muda wako wa Ziada kujiongezea kipato. Njoeni huku mjitajirishe vijana, mshike mkono rafiki yako ili mtoke kimaisha kwa pamoja”, amesema Mohamed.

Aidha, Mohamed alisema kuwa Parimatch inajivunia kuanzisha vitu yenye utofauti wa hali ya juu ukilinganisha na makampuni mengine sokoni.

Program yetu ina tofauti kubwa na makampuni mengine inavyoendesha, sisi tupo katika hali ya kuwasaidia vijana nasio kuwa kandamiza, na ndio maana kwetu hakuna ada ya kujiunga, malipo yapo kwa wakati, mawasiliano yetu ni moja kwa moja kupitia kitengo chetu cha huduma kwa wateja saa 24 siku 7 za wiki”, amesisitiza Mohamed.

Mbali na hilo, Mohamed alisema kuwa Parimatch tokea iingie sokoni imeweza kubadirisha hali ya soko ya zamani ya kubashiri kutoka kwenye kamari hadi kuwa burudani ambapo kila kijana aliyevuka miaka 18 huburudika kwa kubeti na Parimatch ambayo inaongoza hadi sasa kwa kuwa na masoko mengi ya uchaguzi kwa kila mechi.