Jumamosi , 5th Mar , 2022

Ripoti kutoka nchini Ufransa zinadai kuwa Kocha wa PSG Mauricio Pochetino anampango wa kurejea kufundisha soka nchini England baada ya msimu huu kumalizika. Kocha huyo amekuwa akihusishwa kujiunga na Manchester unite lakini kuna uwezekano akarejea katika klabu ya Tottenham.

Maurcio Pochetino

Kwa miezi kadhaa kumekuwa na ripoti kuwa huwenda klabu ya PSG ikaachana na kocha Pochettino endapo kama timu hiyo haitachukua ubingwa wa klabu bingwa Ulaya (Uefa Champions League), lakini pia inadaiwa kocha huyo raia wa Argentina haridhishwi na namna mambo yanavyoendeshwa ndani ya timu hiyo.

Lakini siku chache zilizopita Mkurugenzi wa Ufundi wa PSG Leonardo aliweka wazi kuwa hawana mpango wa kufanya mabadiliko ya benchi la ufundi mwishoni mwa msimu huu hivyo wataendelea kufanya kazi na Pochettino.

Maurcio Pochetino amekuwa akitajwa kwenye orodha ya makocha wanne wanaowaniwa na klabu ya Manchester United kuja kuchukua nafasi ya ukocha mkuu pindi kocha wa muda Ralf Rangnick atakapomaliza muda wake mwishoni mwa msimu na kuchukua majukumu mapya ya kuwa mshauri wa ufundi wa klabu hiyo.

Makocha wengine wanaotajwa kuwa kwenye kinyanganyiro cha ukocha Manchester United ni kocha wa Ajax Erik ten Hag, Carlo Ancelotti wa Real Madrid na kocha wa timu ya taifa ya Hispania Luis Enrique. lakini kwa mujibu wa ripoti kutoka nchini ufaransa hii leo zinadai kuwa Pochetino anatamani kurejea katika klabu ya Tottenham Hot Spur lakini ikitookea ofa ya Manchester United hata kataa.

Pochetino aliifundisha Tottenhama kwa takribani misimu 5 na nusu kati ya mwaka 2014 hadi 2019, ambapo alifanikiwa kukiongoza kikosi hicho kucheza fainali ya Ligi ya mabingwa barani ulaya mwaka msimu wa 2018-19 ambapo walifungwa na Liverpool.