Jumamosi , 7th Jul , 2018

Katika mwendelezo wa mechi za hatua ya 16 bora zinazoendelea mchana huu kwenye viwanja vya Airwing Ukonga jijini Dar es salaam, mpaka sasa timu tatu zimeshafanikiwa kutinga robo fainali huku ushindani wa ponti ukitawala.

Wachezaji wa DMI (Chuichui) kwenye mechi yao dhidi ya Fast Heat (Blue) mapema leo.

Katika mechi tatu ambazo zimeshapigwa hadi sasa timu ambayo imeshinda kwa pointi nyingi ni DMI ambayo imeilaza Fast Heat kwa vikapu 113 dhidi ya 64. Kwa matokeo hayo tayari DMI wapo robo fainali ya Sprite Bball Kings msimu wa 2018 wakiendelea kusogea kwenye milioni 10.

Timu nyingine ni Flying Dribblers ambao wamekuwa moto wa kuotea mbali walipokutana na Ukonga Hitmen wakiwajaza vikpau 87 kwa 63, hivyo kubaki na faida ya vikapu 24 ambavyo vimepelekea robo fainali.

Katika kuisaka robo fainali timu ya St. Joseph nayo haijawa nyuma kwani imehakikisha inatinga hatua hiyo kwa kuwafunga Air Wing vikapu 98 kwa 78 hivyo kujihifadhia faida ya vikapu 20.

Mchezo ambao utakamilisha mechi nne za leo uko mbioni mchana huu kati ya Mbezi Beach KKKT dhidi ya Portland ambayo inaanza muda si mrefu. Baada ya mechi za leo kesho hatua ya 16 bora itaendelea kwa mechi nne kupigwa kwenye uwanja wa Bandari Kurasini.